WAZIRI MKUU:PANUENI WIGO WA MATUMIZI YA GESI ASILIA

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Nishati kuendelea kupanua wigo wa matumizi ya nishati ya gesi asilia ili kupunguza athari za kimazingira zinazotokana na ukataji wa misitu nchini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nishati, January Makamba, kwenye maonesho ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma. Mei 25, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Amesema hayo Mei 25, 2022 wakati alipotembelea maonesho ya Majukumu ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Amesema kuwa Wizara kwa sasa iendelee kupanua wigo wa kufikia Watanzania wengi zaidi katika mikoa mbalimbali nchini. “Tupanue wigo na huduma hii iwafikie watu, tumeanza na Dar es Salaam, tuje kwenye majiji, manispaa zetu na hata hapa Dodoma tuwe na tawi na kazi hii iendelee”
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Shirika la Petroli Tanzania GASPO - TPDC, Injinia. Bartazar Mroso kushoto) wakati akitembelea mabanda, kwenye maonesho ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma. Mei 25, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Aidha, Waziri Mkuu amewataka watendaji wote katika sekta ya nishati kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa nishati ya umeme na nishati nyingine ikiwemo mafuta ili kuendelea kuiwezesha nchi kupata fursa ya kuendelea kukua kiuchumi.

“Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeitaka Serikali kuhakikisha upatikanaji wa umeme katika vyanzo vyetu unaimarishwa, kuendelezwa na kuhakikisha usambazaji wa umeme unawafikia wananchi mpaka vijijini ili kila Mtanzania anufaike kwa kupata nishati hiyo”
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia vipeperushi, wakati akitembelea mabanda, kwenye maonesho ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma. Mei 25, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nishati, January Makamba, wakati alipotembalea banda la Mkoa wa Kigoma, kwenye maonesho ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma. Mei 25, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Maonesho hayo ya siku tatu yaliyoanza Mei 23, 2022 katika viwanja vya bunge yalikuwa na lengo la kuwawezesha Waheshimiwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuuliza maswali kuhusu huduma zinazotolewa na Wizara ya Nishati na taasisi zake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news