Waziri Simbachawene aongoza kikao cha Mawaziri kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu,Mhe. George Simbachawene leo ameongoza kikao cha Mawaziri kwa lengo la kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Wazara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Clarence Ichwekeleza akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika Mei 27, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.George Simbachawene (katikati) akiongoza kikao cha Mawaziri kwa lengo la kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za makazi (wa kwanza kushoto) ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye na mwisho ni Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akichangia hoja wakati wa kikao cha mawaziri cha kujadili taarifa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika Mei 27, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akieleza jambo katika kikao cha mawaziri cha kujadili taarifa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika Mei 27, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Kikao hicho kimefanyika leo Mei 27, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma ambapo kilihudhuriwa na mawaziri wakiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula.

Kikao hicho kimefanyika kama sehemu ya maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 2022 nchini ambapo itakuwa Sensa ya Sita tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na sensa ya watu na makzi hufanyika kila baada ya miaka 10.

Post a Comment

0 Comments