'Wenye bunifu zenu jitokezeni, Serikali ione namna ya kuunga mkono'

NA DIRAMAKINI

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Mei 16,2022 amemwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi, Dokta Hussein Ali Mwinyi, katika Hafla ya Uzinduzi wa Wiki ya Taifa ya Ubunifu pamoja na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka huu wa 2022.
Akizungumza wakati akifungua maonesho hayo mgeni rasmi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman amewataka watu mbalimbali wenye uwezo wa kuonesha bunifu mbalimbali kuendelea kujitokeza ili Serikali ione namna itakavyowaunga mkono.

“Nimeridhika na mambo niliyoona wakati napitia mabanda ya maonesho. Inaonekana kuna hatua kubwa iliyofikiwa katika ubunifu wa bidhaa kwa kutumia teknolojia mbalimbali za kisasa,”amesema.

Hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Kidini na wa Kimila, Vyama vya Siasa, Wananchi, Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Waandishi wa Habari, Wanafunzi, Vikundi vya Burudani, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na Vijana wabunifu.

Pamoja na kuhutubia hafla hiyo, Mheshimiwa Othman aliyeambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, alipata fursa ya kutembelea Mabanda mbalimbali ya Maonyesho ya Ubunifu na pia kupata maelezo ya Wajasiriambali kutoka Ndani na Nje ya Nchi, yakiwemo Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news