'Agosti 23, hakuna atakayeachwa kuhesabiwa,jihandae kuhesabiwa'

NA DIRAMAKINI

WANANCHI wilayani Njombe Mkoa wa Njombe wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha watu wenye ulemavu wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23,2022.

Hayo yamesemwa na Bonfans Hilary ambaye ni Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi katika Halmashauri ya Mji wa Njombe katika vijiji vya Kata ya Luponde wakati wa ziara ya kikazi ya mkuu wa wilaya, Kissa Kafongwa.

Hilary amesema, kitendo cha kuwaficha walemavu wasihesabiwe kinawakosesha haki ya kupata huduma za kijamii.
“Kama una mlemavu ndani wa aina yoyote mtoe ahesabiwe,afahamike ili hesabu yake nayo iingizwe kwenye mipango ya taifa,”amesema Bonifas.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Kissa Kasongwa amesema zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ni muhimu sana katika mipango ya taifa kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Mtaalamu amesema vizuri pia kutakuwa na madodoso mbalimbali naomba sana wote tujitokeze tarehe 23 mwezi wa nane na tutoe ushirikiano ili tuweze kuhesabiwa ili nchi yetu iweze kupanga mipango thabiti ya maendeleo,”amesema DC Kasongwa.

Post a Comment

0 Comments