Waziri Prof.Ndalichako aongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 110 wa Kazi jijini Geneva

GENEVA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameongoza ujumbe wa nchi katika Mkutano wa 110 wa Kazi wa Kimataifa leo Juni 7, 2022 jijini Geneva, Uswisi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kulia) akishiriki Mkutano wa 110 wa Kazi wa Kimataifa Juni 7, 2022 Geneva, Uswisi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Chama cha Waajiri Nchini, Bi. Suzanne Ndomba Doran, Naibu Mkuu wa Kituo Jiji la Geneva, Balozi Hoyce Temu. Kulia ni rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Bw. Tumaini Nyamhokia.

Pia Waziri Ndalichako ameshiriki pia kikao cha kundi la Afrika ambapo ametoa salamu za nchi na kuwaalika nchi wanachama wa Afrika na duniani kote kutembelea nchi ya Tanzania kwa lengo kujionea vivutio vya kitalii na shughuli za ustawi wa wananchi zinazotekelezwa vizuri na Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news