Aiseee!!! Yanga SC waleeeee!!!

NA DIRAMAKINI

JUMAMOSI Yanga SC iliendeleza rekodi ya kutopoteza mechi msimu huu baada ya kutoa sare ya 1-1 na wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchezo uliopigwa dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Mapokezi ya Yanga SC jijini Dar es Salaam leo.
Heritier Makambo alianza kuifungia Yanga dakika ya 40, kabla ya kiungo Mganda, Joseph Ssemunju kuisawazishia Mbeya City kwa penati dakika ya 50 kufuatia nahodha, Bakari Mwamnyeto kuunawa mpira kwenye boksi.

Yanga wanafikisha mechi 29 bila kupoteza mechi, wakiwa tayari mabingwa kwa alama zao 71, nyuma yao wakiwa mabingwa wa misimu minne iliyopita, Simba SC wenye alama 60 za mechi 29 baada ya Tanzania Prisons kuwachapa leo uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Kwa Mbeya City, sare hiyo iliwafanya wafikishe alama 39 baada ya mechi 29 katika nafasi ya tisa.

Katika mchezo huo pia, Yang walikabidhiwa taji la Ligi Kuu ikiwa ni mara ya kwanza kwa misimu minne iliyopita na leo wamewasili jijini Dar es Salaam huku mapokezi yakiwa ya aina yake.

Post a Comment

0 Comments