DCEA:Karibu katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga vita Dawa za Kulevya

NA DIRAMAKINI

KILA mwaka tarehe 26 Juni nchi yetu huungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani. Lengo la Maadhimisho hayo ni kuihamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya.
Mwaka huu shughuli za maonesho kwa ajili ya maadhimisho hayo zinatarajiwa kuanza kesho tarehe 01 Julai 2022 na kufikia kilele siku ya Jumamosi tarehe 02 Julai, 2022 katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam. 

Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi atakuwa Mkuu wa Mkoa Wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makala na na siku ya kilele mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Kauli mbiu ya Maadhimisho haya ni "Tukabiliane na Changamoto za Dawa za Kulevya kwa Ustawi wa Jamii" . Nyote mnakaribishwa kushiriki ufunguzi na kilele cha Maadhimisho haya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news