IGP Sirro:Zoezi la uwekaji alama za mipaka Loliondo linaenda vizuri,msikubali kutumika

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya ziara katika eneo la Loliondo lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kwa ajili ya kujionea zoezi linaloendelea la uwekaji alama za mipaka, ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na kasi iliyopo.
Aidha,IGP sirro amewataka wanasiasa kuacha kuwaamasisha wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo kuleta uvunjifu wa amani.

IGP Sirro ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella, amefanya ziara hiyo leo Juni 13, 2022 ambapo amesema zoezi la uwekaji alama kwenye pori tengefu lililopo Loliondo linakwenda vizuri.

Aidha,IGP sirro amewataka wanasiasa kuacha kuwaamasisha wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo kuleta uvunjifu wa amani.

"Shida kubwa niwaambie ndugu zangu, Watanzania wenzangu, sisi huwa hatugombani hata siku moja, shida kubwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaingilia, wao wana watoto wao wako ulaya wanakula kuku, wanatumia hizi hifadhi zetu kupata faida zao,"amesema IGP Sirro.
Aidha amewaasa wananchi kuwa watulivu nakushirikiana na serikali katika uamuzi huu wenye lengo la kuhifadhi eneo hilo kwa faida mtambuka za nchi.

"Msikubali kutumika kuchochea vurugu ambazo hazina manufaa kwa pande zote na wala msikubali kutumika kwa niaba ya wale wote wasiotutakia mema kama taifa,"amesisitiza IGP sirro

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella alimhakikishia IGP Sirro kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imejipanga kuhakikisha kuwa zoezi linaendeshwa kwa hali ya utulivu kwa kuzingatia sheria za nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news