Iringa rasmi umeme kidigitali

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Queen Cuthbert Sendiga amezindua matumizi ya App ya Nikonekt ambayo inamwezesha mwananchi kuunganishiwa umeme kidigitali.
“Napenda kutoa pongezi kwa TANESCO (Shirika la Umeme Tanzania) mkoani Iringa kwa kuwajali wananchi wake na kuwarahisishia huduma zaidi kwa kuwapa nafasi ya kuunganishiwa na umeme wakiwa na simu yao kiganjani bila kufika katika ofisi za TANESCO kama ilivokuwa awali,"amesema Mheshimiwa Sendiga.

Aidha, mbali na pongezi nyingi alizozitoa Mheshimiwa Sendiga pia alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza miundombinu ya umeme ili kuepusha gharama zisizokuwa za lazima katika kufanya matengenezo.

Post a Comment

0 Comments