Maafisa elimu mkoani Iringa wapigiwa saluti

NA DIRAMAKINI
 
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Iringa, Bi.Happiness Seneda ametoa pongezi kwa maafisa elimu wa wote walipo ndani ya mkoa kwa juhudi mbalimbali walizozifanya ambazo zimeongeza ufaulu ndani ya mkoa.
Pongezi hizo zimekuja wakati mkoa wa Iringa ukishika nafasi ya tatu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2021.

“Hongereni sana nyote kila mmoja kwa nafasi yake. Vile vile pongezi za dhati kwa kuongeza ufaulu bora kwa mtihani wa ki Taifa wa kidato cha nne kutoka asilimia 40.5 mwaka 2020 mpaka asilimia 41.1 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 0.6,”amesema.

Pia amewataka maafisa elimu hao toka halmashauri kuendelea kufanya kazi kwa weledi, kanuni, taratibu na sheria katika kuongeza juhudi ili kuhakikisha Mkoa wa Iringa unashika nafasi ya kwanza kitaifa.

Pia ametumia kikao hicho kuwakumbusha maafisa elimu hao kuwatendea haki watumishi waliochini yao, pamoja kuwa na majibu mazuri kwa watumishi na kutatua kero zao.

"Wapo baadhi ya maafisa hapa wana majibu mabaya sana kwa watumishi na hii inapelekea baadhi ya watumishi kuja kuleta malalamiko mkoani, acheni hiyo tabia, hizi nafasi mpewa kwa neema ya Mungu tu, hivyo watendeeni haki wenzenu,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news