Jambo la Watanzania ni Agosti 23,Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Sensa ya Watu na Makazi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza, Mheshimiwa Amina Makilagi amesema, ni vema viongozi wa dini wakaendelea kuhamasisha waumini wao ili waweze kutambua umuhimu wa Sensa ya Watu ni Makazi Agosti 23,2022 kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anahesabiwa kwenye zoezi hilo.
"Tunaomba viongozi wa dini baada ya ibada muwe mnatoa elimu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa waumini wenu ili waweze kuona umuhimu wa zoezi hili,"amesema Mheshimiwa Makilagi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa, karani wa Sensa atafika katika kaya akiwa na kitambulisho na sare maalumu inayomtambulisha pia ataambatana na kiongozi wa serikali ya mtaa na kitongoji.

Amesema, Sensa ya Watu na Makazi itasaidia Serikali kutimiza wajibu kwa wananchi kulingana na idadi ya watu wa eneo husika pamoja na kupata ufumbuzi wa mahitaji ya watu wenye ulemavu.

Makilagi amesema, Sensa ya Watu na Makazi itasaidia kupata taarifa ya kujua idadi ya wanaume na wanawake,umri,hali ya ndoa(kidemographia),kujua taarifa za kijamii, uchumi, na hali ya mazingira kwa lengo la kupata takwimu sahihi ambazo zitawezesha serikali na wadau wengine kupanga maendeleo ya watu katika sekta mbalimbali za elimu,miundombinu,afya, hali ya ajira na Taifa kwa ujumla.

"Itakapofika saa sita na dakika moja usiku wa kuamkia Agosti 23, mwaka huu watu wote watakaokuwa wamelala ndani ya mipaka yetu ya nchi ya Tanzania wote tutawahesabu naomba mtowe ushirikiano kwa mawakala wa sensa ambao watawatembelea kwenye maeneo yenu,"amesema Makilagi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news