KMC FC:Jambo letu ni kesho, acha Tanzania Prisons waje

NA DIRAMAKINI

KIKOSI cha KMC FC kimekamilisha maandalizi kuelekea katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi Tanzania Prisons ikiwa ni mara baada ya kumalizika kwa mapumziko ya kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Afisa Habari na Mawasiliano KMC FC,Christina Mwagala ambapo amesema,watawakaribisha Tanzania Prisons katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ni mchezo ambao utapigwa saa 16:00 jioni na wachezaji wote wapo tayari kwa mtanange huo.

Amesema,timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana imekuwa na wakati mzuri wa kufanya maandalizi tangu ilipocheza mchezo wa mwisho Mei 19 dhidi ya Mbeya City na kuondoka na ushindi wa magoli matatu kwa bila.

Katika kipindi chote ambacho Timu zilikuwa kwenye mapumziko, KMC iliingia kambini Mei 27 na kuanza program mbalimbali ambapo zimefanyika kwa ufanisi mkubwa ikiwemo kucheza mechi za kirafiki na kwamba hadi sasa Ligi inarejea kila mmoja anafahamu umuhimu wa mchezo huo licha ya kwamba utakuwa na ushindani kutokana na kila timu kuhitaji matokeo.

“Tunakwenda kwenye mechi ngumu na bora, tunafahamu Prisons ni wazuri wanajipanga wasipoteze, lakini kwa upande wa KMC tunajua ubora wa wachezaji wetu tulionao pamoja na benchi la ufundi hivyo tunahitaji kutumia vizuri uwanja wetu wa nyumbani kuzipata alama tatu,"amesema.

“Ligi hivi sasa inakwenda ukingoni na kila mtu anahitaji kutetea nafasi ya kuendelea kuwepo katika msimu ujao, ndio maana tunafahamu ugumu wa mchezo wa kesho, lakini mashabiki wasihofu, timu imeandaliwa vizuri na wajitokeze kutoa sapoti ili kuongeza morali zaidi kwa wachezaji,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news