Kwa nini nipo tayari kuhesabiwa na kutoa taarifa sahihi kuhusu Makazi yangu Agosti 23, 2022?

NA GODFREY NNKO

MIMI tayari nimejiandaa kwa ajili ya kuhesabiwa na familia yangu, ambapo katika Sensa ya Watu na Makazi ya Agosti 23, 2022 nitahakikisha ninashiriki kikamilifu kutoa majibu sahihi kulingana na maswali nitakayoulizwa na karani wa sensa.
Pia, mbali na hayo ili kuiwezesha Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini na Serikali kutekeleza na kufanikisha mipango yake ya maendeleo, nimejiandaa kutoa taarifa zote zinazonihusu kuhusu makazi yangu.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum. 

Kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi. 

Takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo.

Makazi je?

Mkurugenzi Maendeleo ya Makazi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi,Deogratias Kalimenze akielezea msingi wa Sensa ya Majengo anasema kuwa,Sera ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000 katika ibara ya 4.1.8.2 ii)inaelekeza Wizara kuwa na benki ya taarifa za makazi na nyumba.

Lengo ni kusaidia katika maamuzi mbalimbali ya maboresho ya kisekta kwa kujua hali ya makazi, ukuaji wa miji,vifaa vya ujenzi,ujenzi wa nyumba kupitia ushirika,tozo za kodi ya pango la jengo,gharama za ujenzi wa nyumba,mchango wa sekta binafsi katika nyumba,mchango wa serikali katika nyumba na mahitaji ya nyumba.

Pia Bw.Kalimenze anasema,utekelezaji wa Sensa ya majengo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ya Mwaka 2020/2025,ibara7 (d) ambayo imeelekeza Wizara kutambua nakuandaa kanzidata ya nyumba zote nchini kwa kushirikiana na wadau pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya wapangaji na wenye nyumba.

Umuhimu wa Sensa ya Majengo
ITAENDELEA chapisho lijalo

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news