Maandalizi ya Sensa yanakwenda vizuri sana-Kamisaa wa Sensa Makinda


Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Mhe. Anne Makinda amesema maandalizi ya Sensa yanaendelea vizuri ambapo hatua iliyopo sasa ni kuendelea na uelimishaji na uhamasishaji wa wananchi kushiriki Sensa na mafunzo ya Waratibu, Makarani na Wasimamizi wa Sensa katika ngazi zote.
Akizungumza na Waratibu wa Sensa ngazi ya Taifa ambao ndio watafundisha Waratibu wa Sensa ngazi ya mikoa, Kamisaa amesema kazi kubwa ya maandalizi ya Sensa imekamilika na hivyo hatua iliyobaki ni kuendesha mafunzo ya Sensa kwa ngazi za Wilaya hadi Kitongoji,Shehia na Mitaa. (Picha na NBS)

Post a Comment

0 Comments