Mtanzania Novatus Dismas kupewa kandarasi Klabu ya Zulte Weregem

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Zulte Weregem ya Ubelgiji, imetangaza kumsajili kiungo Mtanzania, Novatus Dismas, kutokea Macabi Tel Aviv ya Israel.
Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, ameingia mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu hiyo ambayo imewahi kushinda taji la Belgian Cup mara mbili.

Novatus atakuwa ni mtanzania wa tatu kusajiliwa na timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji "Belgian Jupiler Pro League" baada ya Mbwana Samatta alichezea Royal Antwerp,KRC Genk na Kelvin John ambaye anakipiga kwenye klabu ya KRC Genk pia.

Post a Comment

0 Comments