RC Sendiga:Iringa imetoa Bilioni 4/-kuwezesha wanawake

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Mhe.Queen Sendiga amesema kuwa Serikali ya Mkoa wa Iringa imetoa zaidi ya shilingi bilioni kwenye mfuko wa akina mama wa asilimia nne na wamejipanga kuhakikisha mwaka ujao wa fedha wataongeza zaidi ya hapo.
Mhe. Sendiga amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imefanikiwa kuwatua ndoo wanawake wa Mkoa wa Iringa kwa kuleta miradi mingi ya maji kwenye kila wilaya na halmashauri zake.

Amesema kuwa, Iringa bado kuna changamoto ya ukatili wa kijinsia hivyo serikali ya Mkoa wa Iringa kupitia Polisi na Mahakama imeanza kushughulikia kesi za ubakaji na ulawiti na kisha kuwafunga watuhumiwa wote ambao wamekuwa wanafanya vitendo vya kikatilii.

Pia Mhe.Sendiga amesema kuwa wananchi wa Mkoa wa Iringa waache mara moja tabia ya kuwaficha wananchi ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa sababu nao watashughulikiwa na serikali kama watuhumiwa wengine.

Ameyasema hayo akiwa kwenye baraza la Wanawake la Mkoa wa Iringa ambapo pia limehudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT),Gaudentia Kabaka.

Kwa upande wake, Bi.Kabaka amewapongeza viongozi wa mkoa huo kwa kuendelea kushirikiana kwa ajili ya kuwahudumia wananchi ili kuharakisha maendeleo.

"Nitumie fursa hii kuwapongeza sana Mheshimi Mkuu wa Mkoa,Sendiga na ndugu, Happynes Seneda (RAS) kwa ushirikiano wenu mkubwa wa kazi ambao unathibitisha manafanya kazi nzuri na yenye tija kubwa ndani ya Mkoa wa Iringa, hivyo endeleni kushirikiana nasi kama UWT Taifa tunaziona na tutawasemea vizuri kubwa endeleeni kuchapa kazi huku mkishirikiana na CCM mkoa,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news