Rock City Comedy yatikisa Mwanza, yatoa fursa kwa vijana

NA SAMIR SALUM

MAMIA ya wapenzi wa burudani mkoani Mwanza wamejitokeza katika usiku wa tukio la uchekeshaji liliofanyika katika ukumbi wa New Mwanza Hotel, usiku wa kuamkia leo Jumapili Juni 12, 2022.
Baadhi ya wadau waliohudhuria Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.(Picha zote na Samir Salum, Lango la habari). 

Tukio hilo lililoandaliwa na Jukwaa la Rock City Comedy limepambwa na wachekeshaji mbalimbali wakiwemo Osmond Soka, Amos Comic, Matilda, Sam Comedian, Mbwana Jamal na Tinno huku Mshairi, Mr Romantic akisherehesha katika usiku huo.

Akizungumza mara baada ya tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Rock City Comedy, Julius Muniko amesema kuwa, kuanzishwa kwa Jukwaa hilo ni kutoa fursa kwa vijana kuonesha vijapi vyao na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Muniko amesema, wapo vijana ambao kupitia kikundi hicho wameweza kukuza zaidi vipaji vyao na kupata fursa za kiuchumi katika Warsha mbalimbali hivyo amewaasa vijana wenye kipaji cha kichekesha kujiunga na kikundi hicho.

Awali mmoja wa wachekeshaji, Osmond Soka ameishukuru Rock City Comedy kuwa moja ya sehemu iliyomfanya kuwa mshindi wa tatu katika mashindano ya vipaji kwa wanavyuo ya Uni Talent 2022 na kuondoka na Fedha taslimu shilingi milioni moja.
Aidha, Soka amewaomba wadau mbalimbali pamoja na Serikali kujitokeza kudhamini Jukwaa la Rock City Comedy ili kuwawezesha kuendesha Matukio mbalimbali kwa ajili ya kutoa Burudani na kukuza fursa za kiuchumi kwa vijana wanaojiunga na jukwaa hilo.
Baadhi ya wadau waliohudhuria Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Cheko si haba ndani ya Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Baadhi ya wadau waliohudhuria Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mchekeshaji Sawe boy Akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mchekeshaji Akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Baadhi ya Wadau waliojitokeza katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mshairi Mr Romantic akisherehesha katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mshairi Mr Romantic akitumbuiza katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.

Mchekeshaji Amos Comic Akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mchekeshaji Akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel
Baadhi ya Wadau waliojitokeza katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mchekeshaji Sam Comedian Akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mchekeshaji Osmond Soka aliyekuwa mshindi wa tatu katika mashindano ya vipaji kwa wanavyuo ya Uni Talent 2022 akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news