Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga lafana, Barrick yanogesha

NA KADAMA MALUNDE

KATIKA mipango yake ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kukuza sekta ya utalii nchini, kampuni ya Barrick kupitia mgodi wa Bulyanhulu, imekuwa moja ya wadhamini wakuu wa Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga lililofanyika katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa-Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Akina mama kutoka Kishapu wakitwanga nafaka kwenye tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga.(Picha na Malunde 1 blog).

Mbali na ufadhili kampuni iliwezesha ufungaji wa vifaa kwa ajili ya kuwawezesha wananchi waliohudhuria kwenye tamasha hilo kubwa kuweza kuona filamu maarufu ya kukuza utalii nchini ijulikanayo kama The Royal Tour, iliyomshirikisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Burudani ya Ngoma ya Wagoyangi wanaocheza na nyoka ikiendelea kwenye tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga.

Tamasha hilo lilizinduliwa Juni 6,2022 na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na kufungwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema Juni 7,2022.
Kaimu Meneja wa Mahusiano na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu Zuwena Senkondo (kushoto) akiwa na wafanyakazi wenzake baada ya kupokea cheti cha shukrani kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Sophia Mjema, (katikati) kutokana na kampuni hiyo kuunga mkono Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa kufunga Tamasha hilo, Mhe. Mjema amewapongeza na kuwashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki tamasha la utamaduni ili kutii na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha kila Mkoa unaenzi na kudumisha tamaduni zao hivyo kuwakumbusha wananchi kuenzi tamaduni zao kama Rais Samia anavyosisitiza mara kwa mara juu ya umuhimu wa kuenzi utamaduni zikiwemo mila na desturi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana (katikati) akizindua Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma cha Butulwa Old Shinyanga kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga. Kushoto aliyevaa tisheti nyeupe ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.
Wananchi wakiwa kwenye tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Skrini kubwa iliyoletwa na Kampuni ya Barrick katika kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa Old Shinyanga kwa ajili ya kuonesha Filamu ya The Royal Tour. Wananchi waliohudhuria kwenye tamasha hilo kubwa walipata fursa ya kuona filamu ya kukuza utalii nchini ijulikanayo kama The Royal Tour, iliyomshirikisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wakiwa kwenye tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Sophia Mjema wakati akifunga Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga Juni 7,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick katika Tamasha la Utamaduni mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Meneja wa Mahusiano na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo (kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news