Mbunge wa Jimbo la Kwela ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ametaka watumishi wa umma wote wanaodaiwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za mradi wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mfinga kufikishwa mahakamani haraka baada ya kubainika kuwepo kwa viashiria vya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Akizungumza Julai 19,2026 baada ya kukagua mradi huo wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kuhamasisha shughuli za maendeleo katika Jimbo la Kwela, na kueleza kuwa hajaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo licha ya fedha nyingi zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wake.

Ameeleza kuwa kati ya shilingi milioni 220.1 zilizotolewa kwa mradi huo tangu Julai 2025, tayari shilingi milioni 212.9 zimetumika lakini ujenzi bado haujakamilika jambo ambalo linaibua maswali kuhusu uwajibikaji na usimamizi wa fedha za umma.

Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo