TANESCO yaanza kutoa huduma kidigitali mkoani Shinyanga

NA KADAMA MALUNDE

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limezindua rasmi Mfumo rahisi wa maombi ya huduma ya Umeme kwa njia ya Mtandao ‘Kidigitali’ maarufu NI- KONEKT huku likiwaomba wananchi kuchangamkia fursa hiyo ambayo inamrahisishia mteja kupata huduma za umeme bila kufika katika ofisi za TANESCO.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga wakiendelea kuhudumia wateja wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa NI- KONEKT leo Jumatatu Juni 6,2022.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga wakigonga Cheers wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa NI- KONEKT leo Jumatatu Juni 6,2022.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatatu Juni 6,2022 katika ofisi za TANESCO Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa pia na wateja wa TANESCO waliofika kupata huduma za umeme.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Ni – Konekt, Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Kurwa Mangara amesema Mfumo wa Ni- Konekt unamuwezesha mteja kutuma na kufuatilia maombi ya umeme kwa njia ya kidigitali, kutoa taarifa za dharura, kufanya maombi yasiyo ya umeme kutoa malalamiko pamoja na kufanya maulizo mbalimbali.
Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Kurwa Mangara na mteja wa TANESCO Esther Makoye wakikata keki wakati wa uzinduzi wa Mfumo rahisi wa maombi ya huduma ya Umeme kwa njia ya Mtandao ‘Kidigitali’ maarufu NI- KONEKT leo Jumatatu Juni 6,2022.

“Kupitia mfumo huu wateja wetu watapata huduma ya umeme kwa urahisi na haraka huko waliko wakiwa wanaendelea na shughuli zao, kila kitu kitafanyika kwa njia ya digitali. Huduma hii inarahisisha sana kwa wafanyabiashara wanaohitaji huduma zetu. Pia itapunguza manung’uniko mbalimbali na mianya ya rushwa na vishoka..Ukiomba maombi SMS itakuja, hatua tutakazokuwa tunazifanya SMS itakuja kwa hiyo utakuwa unajua kila hatua inayoendelea”,amesema.

Mhandisi Mangara amesema ili mteja/mwombaji aweze kupata huduma ya maombi ya umeme kupitia mfumo wa Ni- konekt anapaswa kuwa na kitambulisho cha Taifa (NIDA) huku akieleza kuwa Mfumo huo unatumia njia kuu tatu kufanya kazi yaani maombi kupitia Kiswaswadu (USSD Code), Tovuti (Web portal) na Programu tumishi (Nikonekt Mobile App).
Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Kurwa Mangara akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo rahisi wa maombi ya huduma ya Umeme kwa njia ya Mtandao ‘Kidigitali’ maarufu NI- KONEKT leo Jumatatu Juni 6,2022.

Ameeleza kuwa mteja anaweza kutumia mfumo wa Nikonekt kwa kutumia njia ya Tovuti (Web portal) ya www.tanesco.co.tz ambapo mteja anaweza kutumia simu janja, komputa au kifaa kingine chenye uweo wa Intaneti.

“Njia zinazotumika kupata mfumo wa Ni- konekt ni pamoja na kutumia namba maalumu za USSD Code (Kiswaswadu) kwa kupiga namba *152*00# kwa watumiaji wa simu za kawaida. Bonyeza *152*00#, nenda namba 4 (Nishati) kisha nenda tena namba 4 (TANESCO) baada ya hapo nenda namba 1 (Maombi ya umeme) baada ya hapo utaulizwa unahitaji kwa matumizi ya nyumbani/biashara/taasisi…Kila hatua unayofanya utakuwa unapatiwa Ujumbe (SMS) kwenye simu yako”,amesema Mhandisi Mangara.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Mfumo rahisi wa maombi ya huduma ya Umeme kwa njia ya Mtandao NI- KONEKT.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga na wateja wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Mfumo rahisi wa maombi ya huduma ya Umeme kwa njia ya Mtandao NI- KONEKT.

Amesema njia nyingine ya kutumia mfumo wa Ni- konekt ni kupitia Ni-konekt Mobile App ambapo mteja anaweza kupakua Programu ya Ni- konekt kwenye simu yenye uwezo wa Intaneti ambapo App ya Ni-Konekt inapatikana kwa watumiaji wote wa simu janja (Smartphone). Kwa watumiaji wa Android , Aplikesheni ya Nikonekt inapatikana kwenye Play store na App store kwa watumiaji wa Iphone.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga wakiwa wameshikamana 'Wame Konekt' wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa NI- KONEKT leo Jumatatu Juni 6,2022.

Nao wananchi akiwemo Esther Makoye mkazi wa Viwanja vya Mwadui Mjini Shinyanga wameipongeza TANESCO kuanzisha mfumo wa Ni – Konekt ambao amesema utawapunguzia wananchi muda na gharama za kufuata huduma za umeme katika ofisi za TANESCO.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news