Barrick Bulyanhulu na North Mara wafanya jambo kubwa Siku ya Mazingira

NA DIRAMAKINI

KATIKA kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani 2022 mwaka huu,Wafanyakazi wa Migodi wa Barrick Bulyanhulu na North Mara, walishiriki zoezi la kusafisha maeneo mbalimbali ya wananchi wanaoishi jirani, shule na hospitali pia migodi ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali vya usafi na kutoa elimu ya kulinda migodi na kutunza Mazingira kwenye jamii.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu wakishiriki kusafisha maeneo ya mtaa wa Kakola katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani pia mgodi ulitoa msaada wa vifaa mbalimbali vya usafi kwa kata ya Bulyanhulu.

Mgodi wa North Mara pia uliandaa mechi ya soka ya kushindania Ng’ombe iliyozikutanisha timu za Nyamongo Fc na Tarime Fc, iliyovutia mamia ya wakazi wa maeneo ya jirani wakiongozwa na wenyeviti 11 wa vijiji ,ambapo Tarime FC iliibuka kidedea na kukabidhiwa zawadi hiyo na Afisa Mazingira wa Wilaya ya Tarime,Martha Mahule ambaye alikuwa ni mgeni rasmi.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali baada ya kukamilisha zoezi la kusafisha Mazingira
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu wakishiriki kusafisha maeneo ya mtaa wa Kakola katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani pia mgodi ulitoa msaada wa vifaa mbalimbali vya usafi kwa kata ya Bulyanhulu.

Kauli mbinu ya Siku ya Mazingira mwaka huu nchini ni "Tanzania ni Moja tu,Tuyatunze Mazingira".
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu wakishiriki kusafisha maeneo ya mtaa wa Kakola katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani pia mgodi ulitoa msaada wa vifaa mbalimbali vya usafi kwa kata ya Bulyanhulu
Wafanyakazi wa North Mara wakiwa na Wanafunzi wa sekondari ya Nyamongo baada ya kufanya usafi na kukabidhi vifaa kwa shule hiyo.
Wachezaji wa Namungo FC na Tarime Fc wakichuana vikali katika mechi ya kirafiki ya kuadhimisha Siku ya Mazingira
Timu ya Tarime FC ikikabidhiwa zawadi ya Ng'ombe baada ya kuibuka kidedea
Meneja Mazingira wa North Mara,Frank Ngoroma akielezea umuhimu wa kutunza Mazingira.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news