Viongozi na wadau wa Skauti wakutana, Waziri Mkenda atangaza Siku ya Mkutano Mkuu

NA MATHIAS CANAL, WEST

MKUTANO Mkuu wa SKAUTI umepangwa kufanyika Julai 2, 2022 jijini Dodoma ukiwa na ajenda kubwa ya uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa kuendelea kuhudumu katika nafasi mbalimbali.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof Adolf Mkenda amyeyasema hayo leo Juni 3, 2022 jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa pamoja wa mashauriano wa viongozi na wadau waandamizi wa Skauti nchini.
Mkutano huo kwa kauli moja umekubaliana kuundwa kamati ya pande zote mbili za muungano ili ili kuwa na mapendekezo yatakayoweza kuboresha uratibu na shughuli za Skauti ikiwa ni pamoja na kamati hiyo kutoa mapendekezo kwenye Bodi itakayochaguliwa kwenye uchaguzi mkuu baada ya Bodi iliyokuwepo kumaliza muda wake.

Waziri Mkenda ameeleza kuwa Bodi hiyo itakapochaguliwa itakuwa na jukumu la kushauri namna bora ya kuratibu na kuendesha shughuli za Skauti.
Kuhusu changamoto za kikatibu kuhusu Zanzibar kwenye uendeshaji wa Skauti, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda amesema kuwa atashauriana na Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar.

Naye Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Mhe Lela Mohamed Mussa amempongeza Waziri Mkenda kwa kupanga kikao hicho cha mashauriano ambacho kimetoa muelekeo.

Amewasihi wajumbe na wanachama wote wa SKAUTI Tanzania kujitayarisha kwa ajili ya mkutano huo wa uchaguzi.
Amesema kuwa, miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na nafasi ya Zanzibar katika masuala ya SKAUTI.

Mhe. Lela amewasihi wanachama wote kusimama imara na kuendeleza ukakamavu kwani SKAUTI ni chama chenye heshima kubwa na kioo cha jamii nchini kuwalea watoto kuanzia utotoni ili kuwa katika malezi bora ya uzalendo na uwajibikaji.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Ali Abdullgulam Hussen, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ndg. Ali Khamis Juma, Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Lyabwene Mtahabwa, Skauti Mkuu Tanzania, Mhe. Mwantumu Mahiza na Askofu Mkuu wa Jimbo la Mbeya na Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Skauti, Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news