DCEA yapitisha msako dhidi ya dawa za kulevya hadi uvunguni mwa vitanda, Kamishna Jenerali Kusaya asema ole wao

NA GODFREY NNKO

NESI msaidizi anayehudumu katika Zahanati ya Kariakoo (Kariakoo Dispensary) iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Bw. Salum Shabani Mpangula (54) amekamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) akiwa na kilogramu 174.77 za dawa za kulevya aina ya heroine nyumbani kwake.
Hayo yamesemwa leo Juni 3, 2022 na Kamishana Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha Januari hadi Mei,2022.

Amesema kuwa, mtuhumiwa alikamatiwa nyumbani kwake eneo la Tabata Relini lililopo Halamshauri ya Wilaya ya Ilala jiini Dar es Salaam.

"Mei 12, 2022 katika eneo la Tabata Relini Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ilikamata kilogramu 174.77 za dawa za kulevya aina ya heroine.

"Katika tukio hilo Salum Shabani Mpangula mwenye umri wa miaka 54,mkazi wa Relini Tabata ambaye ni nesi msaidizi Kariakoo Dispensary amekamatwa kwa kusafirisha dawa hizo,"amesema Kamishna Jenerali Kusaya.

Amefafana kuwa,mtuhumiwa alikamatwa kufuatia upekuzi uliofanywa nyumbani kwake. "Pakiti 162 zenye unga uliodhaniwa kuwa dawa za kulevya zilikutwa ndani ya viroba sita vilivyokuwa vimehifadhiwa chumbani kwa mtuhumiwa, na pakiti moja ya unga huo ilikuwa imewekwa kwenye mfuko mweusi wa nailoni na kufichwa chini ya kitanda,"amesema.

Kamishna Jenerali Kusaya amesema kuwa, taarifa za uchunguzi wa kitaalam kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali zimethibitisha kuwa pakiti zote 163 zilikuwa na dawa za kulevya aina ya heroine ambazo jumla yake ni kilogramu 174.77 na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za kisheria kukamilika,"amesema.

Mfumo

Wakati huo huo Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imesema kuwa, kupitia Mfumo wa Kielektroniki (PEN-ONLINE SYSTEM) imefanikiwa kuzuia uingizwaji wa kilogramu 122,047.085 na lita 85 za kemikali bashirifu.

"Kwa upande wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya, mamlaka inaendelea kufanya kaguzi za kufuatilia watu wanaokiuka taratibu za uingizaji na usambazaji wakemikali bashirifu na dawa hizo ili kuzuia uchepushwaji,"amesema.

"Katika kipindi hicho, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekamata jumla ya kilogramu 877.217 za dawa za kulevya na kuzuia uingizwaji wa kilogramu 122,047.085 na lita 85 za kemikali bashirifu nchini.

"Dawa zote hizo ni heroine kilogramu 174.112 ziliohusisha watuhumiwa wawili na bangi kilogramu 703.105 zilizohusisha watuhumiwa sita ambao wote wamefikishwa mahakamani,"amesema.

Kamishana Jenerala Kusanya amesema kuwa, mamlaka hiyo imeteketeza hekari 21 za mashamba ya bangi mkoani Arusha zikiwwemo kilogramu 250.7 za dawa za kulevya aina ya heroine na cocaine ambazo mashauri yake yalimaliika mahakamani.

Amesema, uteketezaji wa dawa hizo ulifanyika katikakiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara kwa utaratibu maalum ambao uwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari.

Pia amesema, katika kuhakikisha jamii inapata elimu sahihi juu ya tatizo la dawa za kulevya wameandaa muongozo utakaotumika kutoa elimu.

Aidha, mamlaka imeshiriki kuandaa ujumbe juu ya tatizo la dawa za kulevya katika Mbio za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea na kutoa elimu kwa Kamati za Ulinzi na Usalama, kamati za afya na watendaji wa Serikali za Mitaa ili wasaidie kuongeza uelewa wa tatizo la dawa za kulevya kwa jamii.

"Tuendelee kupeana ushirikiano hawataingiza iwe kwa nchi kavu, angani au baharini. Serikali ina mkono mrefu sana na popote unafika,"amesema.

Post a Comment

0 Comments