Wafanyabiashara kutoka Tanzania watakiwa kusitisha kununua mahindi nchini Malawi hadi Ubalozi utakapowapa mrejesho, ni baada ya Malawi kusitisha uuzaji wa mahindi nje

NA DIRAMAKINI

UBALOZI wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania nchini Malawi umesema kuwa, Serikali ya Malawi imesitisha kuuzwa kwa mahindi nje ya nchi kutokana na mashaka ya kuwa na upungufu wa chakula.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malawi, Mheshimiwa Humphrey Polepole kwenda kwa wafanyabiashara wa mazao hapa nchini.

Balozi Polepole amesema Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malawi unafuatilia suala hilo kwa karibu huku ukiwataka wafanyabiashara kusitisha mpango wa kununua mahindi nchini Malawi mpaka Ubalozi utakapotoa taarifa nyingine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news