Waziri Mkuu kushuhudia zoezi la Awamu ya Pili ya wananchi 117 kutoka kaya 27 wanaohama kwa hiari yao wenyewe kutoka Ngorongoro kuelekea Kijiji cha Msomera

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 23, 2022 anafanya ziara ya siku moja katika mkoa wa Arusha na Tanga ambapo atashuhudia zoezi la Awamu ya Pili ya wananchi takribani 117 kutoka kaya 27 wanaohama kwa hiari yao wenyewe kutoka katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuelekea kijiji cha Msomera, Handeni.
Mheshimiwa Majaliwa pia atakagua Makazi na miundombinu ya huduma kwa wananchi katika kijiji cha Msomera, Handeni mkoani Tanga.
Pia Mheshimiwa Majaliwa atakagua alama zilizowekwa kubainisha eneo la hifadhi ya pori tengefu la Loliondo la Kilometa za mraba 1500.
Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza wakazi hao kwa maamuzi yao ya kuhamia Katika kijiji cha Msomera ambapo amewahakikishia kwamba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia. Suluhu Hassan ipo pamoja nao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news