WHI inajenga nyumba za gharama nafuu kuwakopesha watumishi-Waziri Mhagama

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema Watumishi Housing Investment (WHI) inajenga nyumba bora za gharama nafuu kwa ajili ya kuwakopesha na kuwauzia watumishi wa umma, ikiwa ni utekelezaji wa kipaumbele cha Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan cha kutatua changamoto ya makazi kwa watumishi wa umma nchini.
Mhe. Jenista amesema hayo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukakua utekelezaji wa miradi ya nyumba zinazojengwa na Watumishi Housing Investment (WHI) katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments