Aisee!!! Yanga SC wanakomba kila kitu,Coastal Union wajisalimisha wenyewe

NA DIRAMAKINI

LICHA ya mshambuliaji wa kikosi cha Coastal Union, Abdul Seleman maarufu Sopu kufunga mabao matatu katika mchezo wa fainali wa michuano ya Azam Sports Federation Cup Tanzania bara uliochezwa jijini Arusha, kwa Yanga SC hawakutetereka.
Katika mchezo huo wa fainali kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga timu hizo zimefanikiwa kutoka sare ya kufungana mabao 3-3 ambapo mabao ya Yanga yakifungwa na Salum Abdalah (Fei Toto) bao la pili likifungwa na mshambuliaji mkongomani Makambo na bao la tatu la Yanga likifungwa na Denis Nkane na kukamilisha dakika 120 kwa kufungana mabao 3-3.

Dakika 90 zilimalizika kwa kufungana mabao 2-2 na kuongezwa dakika 30.

Mikwaju ya penati Yanga wamefanikiwa kufunga penati 4 na Coastal Union wakifunga Penati 1 pekee.

Katika mtanange huo, mfungaji bora wa michuano hiyo ni Abdul Seleman Sopu ambapo amefikisha jumla ya mabao tisa.

Post a Comment

0 Comments