Ajali iliyohusisha gari, mkokoteni yaua saba jijini Dodoma

NA DIRAMAKINI

WATU saba wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Landcruiser yenye namba za usajili STL 9534 mali ya Idara ya Maji Mkoa wa Katavi.

Ni baada ya gari hilo kugonga kwa nyuma mkokoteni uliokuwa unavutwa na ng’ombe katika Kijiji cha Lugala- Kata ya Manzase Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Ajali hiyo imetokea leo Julai 3, 2022 saa 11 alfajiri wakati gari hiyo ikitokea Dodoma kuelekea Mtera kugonga mkokoteni huo uliokuwa ukikokotwa na ng’ombe wawili huku ukiwa umepakia abiria 12.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea ajali hiyo na kubainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa gari hiyo.

Amesema, mbali na watu hao saba, pia ng’ombe wawili waliokuwa wakikokota mkokoteni huo nao pia wamefariki kutokana na ajali hiyo.

Amesema, gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Paschal Sitta mkazi wa Katavi, alikuwa akiendesha gari hiyo kwa mwendokasi ambao ulimsababisha kushindwa kung’amua iwepo wa mkokoteni huo mbele yake kwa haraka.

Pia amesema, majeruhi watano wa ajali hiyo wamewahishwa katika hospitali ya General mkoani Dodoma kwa ajili ya matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news