Rais Dkt.Mwinyi amshirikisha fursa za uwekezaji Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora duniani

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora (Dawoodi Bohoras) duniani, Syedna Muffaddil Saifuddin na kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa dhehebu hilo kuja kuwekeza Zanzibar.
Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu jijini Zanzibar ambapo kiongozi huyo wa Madhehebu ya Bohora (Dawoodi Bohoras), akiwa na ujumbe wake walionesha azma ya kuendedelea kumuunga mkono Rais Dkt.Mwinyi katika juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt.Mwinyi amemueleza kiongozi huyo fursa mbalimbali zilizopo Zanzibar pamoja na mazingira mazuri yaliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anayoiongoza katika biashara na uwekezaji.
Rais Dkt.Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa dhehebu hilo kubwa duniani kuja kuekeza Zanzibar na kuwahakikishia kwamba Serikali imeweka mikakati madhubuti sambamba na mashirikiano makubwa.

Post a Comment

0 Comments