Ajali ya lori, coaster yaua watano Mbeya

NA MWANDISHI WETU

WATU watano wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya lori la mizigo lililobeba shehena ya mahindi kufeli breki na kugonga gari dogo la abiria aina ya Coaster lililokuwa likitoka Mbeya Mjini kwenda Wilaya ya Mbarali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Urlich Matei amesema kuwa, ajali hiyo imetokea Julai 5, 2022 kwenye mteremko mkali wa barabara kuu ya Mbeya-Dar es Salaam

Amesema kuwa, lori la mizigo lililokuwa na tela liligonga gari la abiria na kisha kuliburuza mpaka kwenye vibanda vilivyopo pembezoni mwa barabara na kusababisha vifo hivyo na majeruhi.
''Gari lililosababisha ajali lilitokea Mkoa wa Songwe kwenda jijini Dar es Salaam huku likiwa limebeba shehena za mahindi na chanzo cha ajali ni kufeli breki kutokana na mteremko mkali ambao alishindwa kulimudu,''amesema Kamanda Matei.

Kamanda Matei amesema, miili ya watu waliofariki kwenye ajali hiyo imehifadhiwa kwenye kituo cha afya cha Inyala huku majeruhi wakipelekwa Hosptali ya Wilaya ya Igawilo ya Mbeya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news