Balozi wa Kodi Subira Khamis Mgalu:Elimu ya mlipa kodi imekuwa na matokeo mazuri

NA DIRAMAKINI

BALOZI wa kodi nchini, Mheshimiwa Subira Khamis Mgalu amesema kupitia elimu inayotolewa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imesaidia kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini.

Balozi Subira ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la TRA wakati wa maonesho ya biashara ya kimataifa 46 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere.

Amesema, elimu inayotolewa na TRA imefumbua macho wawekezaji juu ya elimu ya mlipa kodi na kuja kuwekeza nchini.

"Wananchi wamejitokeza zaidi katika Mamlaka ya Mapato pamoja na wawekezaji wemejitokeza kupata elimu ya mlipa kodi na baada ya maelezo hayo wawekezaji wamevutiwa kuwekeza nchini kwetu hili linakwenda sambamba na mpango wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema.
Vilevile amesema kuwa, kwenye idara ya sera na utafiti ya mamlaka hiyo itakuwa ikitafiti namna ya kuongeza walipa kodi na kupunguza walipa kodi wachache wanaolipa kodi nyingi.

Aidha, ametoa wito kwa watanzania kudai risiti kwa kila manunuzi huku wafanyabiashara wakitoa risiti kwa kila wanapofanya mauzo.

Ameongeza kuwa,mamlaka hiyo imepewa lengo la kukusanya kiasi cha shilingi Trilioni 23 na kwamba pesa hizo ndio zitakazojenga miradi mbalimbali ya kimkakati na elimu bure, pamoja na utoaji wa huduma za afya na miundombinu mbalimbai nchini.

Post a Comment

0 Comments