Bosi wa Yanga SC aomba kuondoka, kamati yaridhia

NA DIRAMAKINI

KAMATI ya Utendaji ya Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imeridhia kwa kauli moja pendekezo la Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Bw.Senzo Hammilton Mazingiza la kutoongezewa mkataba wake unaoishia Julai 31, 2022.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 30, 2022 na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu ya Yanga jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo imefikiwa baada ya kamati hiyo kufanya kikao chake cha kwanza cha Kikatiba leo Julai 30,2022 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam chini ya Rais wa klabu hiyo, Mhandisi Hersi Ally Said.
Agosti 31, 2021 Senzo ambaye ni raia wa Afrika Kusini alitangazwa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo.

Senzo alitangazwa huku akikabidhiwa jukumu la kusimamia mchakato wa mabadiliko kufikia mwisho. Awali alikuwa mshauri mkuu wa Yanga kuelekea kwenye mabadiliko baada ya kubwaga manyanga ndani ya Simba SC ambapo alikuwa kwenye nafasi hiyo.

Post a Comment

0 Comments