BRANCH yadhamiria kutoa mikopo kwa Watanzania papo kwa papo

NA DIRAMAKINI

KAMPUNI ya Branch inayoongoza duniani kwa utoaji mikopo kwa watu binafsi kwa njia ya simu za mikononi, imeelezea nia yake thabiti ya kuwafikishia huduma za kifedha za gharama nafuu mamilioni ya Watanzania popote pale walipo.
Msimamizi wa Huduma kwa wateja wa Kampuni ya Kutoa mikopo kwa njia ya simu za mkononi kupitia App ya Branch, Reuben Wanyamawi akiongea na wanahabari jijini Dar es Dalaam juu ya mpango wa kampuni hiyo kuwafikia Watanzania wengi zaidi.

Tangu kuanzishwa kwake hapa nchini mwaka 2015, Branch tayari imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 73 na kuwafikia zaidi ya watu milioni moja na laki tano walipo sehemu mbali mbali.

Mikopo ainayotolewa na Branch kupitia App yao inaanzia kiasi cha shilingi 5,000 hadi shilingi 1,000,000.
Msimamizi wa Huduma kwa wateja wa Kampuni ya Kutoa mikopo kwa njia ya simu za mkononi kupitia App ya Branch, Reuben Wanyamawi akiongea na wanahabari jijini Dar es Dalaam juu ya mpango wa kampuni hiyo kuwafikia Watanzania wengi zaidi.

Akiongea na wahariri wa vyombo vya Habari, msimamizi wa huduma kwa wateja kwa Tanzania Reuben Wanyamawi, alisema Branch imejipanga vyema kuwafikishia huduma za mikopo Watanzania popote pale walipo na muda wowote hivyo kuwezesha kutatua changamoto zao zinazohitaji fedha.

“Branch inayofuraha kuwahudumia Watanzania na mkakati wetu ni kuwafikia Watanzania wengi zaidi popote pale walipo na muda wowote. Ni jambo la kuvutia kuona kuwa idadi ya watu wanaotumia huduma zetu imekuwa ikiongezeka kila kukicha,”alisema.
Msimamizi wa Huduma kwa wateja wa Kampuni ya Kutoa mikopo kwa njia ya simu za mkononi kupitia App ya Branch, Reuben Wanyamawi (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya Pamoja na wanahabari jijini Dar es Dalaam, muda mfupi baada ya kuelezea mpango wa kampuni hiyo kuwafikia Watanzania wengi zaidi. 


“Tunaamini kuwa kila mtu popote pale lipo anahitaji na anastahili huduma za kifedha. Kuongezeka kwa matumizi ya simu janja kunaongeza fursa kwa watu wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha,”aliongeza.

Kwa mujibu wa msimizi huyo wa huduma kwa wateja, inachukua dakika chache tu kwa mtu kuomba mkopo na kuupata kupitia App ya Branch. “Ukishathibitishwa, inachukua dakika chache tu kupata mkopo wako. Tunatumia taarifa zilizopo kwenye simu za wateja kufanya maamuzi ya kutoa mikopo. Kama ombi lako halijakubaliwa, usijali. Wakati mwingine huchukua mara kadhaa kuomba ndiyo mteja apate mkopo,” alisema.

Katika kuhakisha wateja wanafurahia huduma zao alisema, Branch ina utaratibu wa rufaa ambapo kama mteja akimshawishi mteja mwingine kuchukua mkopo na akaulipa kwa wakati, mteja huyo atapata zawadi ya shilingi 7,000 na mteja mpya atapata zawadi ya shilingi 7,000 pia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news