Tanzania Commercial Bank yazindua tawi jipya Bukoba

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mhe. Moses Machali (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank lililozinduliwa katika Wilaya hiyo hivi karibuni ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuhakikisha inawafikia wateja wake kila kona ya nchi. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial, Sabasaba Moshingi, Mkurugenzi Rasilimali watu, Diana Myonga pamoja na Mkurugenzi wa Mikopo, Henry Bwogi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Benki hiyo lililozinduliwa katika Wilaya ya Bukoba hivi karibuni ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuhakikisha inawafikia wateja wake kila kona ya nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mhe. Moses Machali akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Sabasaba Moshingi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Benki hiyo mara baada ya uzinduzi wa Tawi hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news