Cha kwanza nataka kuona mnajitambulisha kwa vipaji vyenu na si ulemavu wenu-Dkt.Abbasi

NA DIRAMAKINI

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi jijini Dar es Salaam, amekutana na wasanii mchanganyiko wa muziki wanaounda Jumuiya Band na kuwapa miongozo mbalimbali. Wasanii hao ambao ni mchanganyiko wa walemavu na wasio walemavu, walifika kumuona kiongozi huyo ili kupata miongozo mbalimbali ya kuendeleza kundi lao. 
“Cha kwanza nataka kuona mnajitambulisha kwa vipaji vyenu na si ulemavu wenu. Ukweli kwamba mmeungana na mnatunga nyimbo mbalimbali maana yake ninyi mnavipaji sasa mjiamini, mjitambulishe na mjitangaze kwa vipaji hivyo na si hali yenu,” alisema Dkt. Abbasi huku wasanii hao wakieleza kufurahishwa na mageuzi mbalimbali yanayofanywa kwenye sekta ya sanaa nchini chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan na Wizara chini ya Waziri Mohammed Mchengerwa.

Post a Comment

0 Comments