Dkt.Msolla asema anastaafu Jumapili Yanga SC, lakini...

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga,Dkt.Mshindo Msolla amesema,akistaafu Jumapili ya wiki hii katika nafasi hiyo ya uwenyekiti ataendelea na ajenda zake mbili.
Ameyasema hayo leo Julai 4, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kupitia mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam ambao umetoa taarifa rasmi kuwa, Uchaguzi Mkuu utafanyika Julai 9, 2022 badala ya Julai 10, iliyotarajiwa awali.

"Mimi binafsi nitaendelea na ajenda kuu mbili baada ya kustaafu Jumapili, la kwanza nitahamasisha umoja nchi nzima na la pili nitaendelea kuhamasisha mashabiki wetu waendelee na usajili.

"Aliyechukua fomu ya Urais ana uwezo mkubwa wa kuendeleza kile ambacho tulikianzisha, nitaendelea kumuunga mkono na kuzunguka nchi nzima na wenzangu kuhamasisha umoja wa klabu yetu,"amesema Dkt.Msolla

Post a Comment

0 Comments