Azam FC yaanza kuingia kandarasi za kibabe

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Azam FC imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao baada ya kumsajili Mfungaji Bora wa Azam Sports Federation Cup (ASFC), Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ kutoka Coastal Union kwa mkataba wa miaka mitatu.
Sopu anakuwa mchezaji mpya wa nne na wa pili tu mzawa, baada ya kiungo mshambuliaji, Cleophace Mkandala kutoka Dodoma Jiji pamoja na wageni watatu, viungo washambuliaji, Kipre Junior na Tape Edinho kutoka Ivory Coast na kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala.

Usajili wa safari hii ukifanywa na mmiliki wa timu mwenyewe, Yussuf Bakhresa kwa kushirikiana na Mtendaji Mkuu, Abdukkarim Amin (Popat). 
Azam FC imeimarisha benchi la ufundi kwa kumrejesha aliyewahi kuwa mchezaji na kocha wake Msaidizi, Kali Ongala safari hii akipewa jukumu la kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili huku ikiajiri kocha mpya wa makipa, raia wa Hispania, Dani Cadena ambaye amewahi kufundisha klabu za Sevilla na Real Betis za Hispania na nyingine za China na Asaudi Arabia akiwa na uzoefu mkubwa na elimu ya juu ya Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news