Yanga SC yapuliza filimbi kwa wagombea, yafunga pazia matawini

NA DIRAMAKINI

WAGOMBEA uongozi katika Klabu ya Yanga yenye maskani yake jijini Dar es Salaam wametakiwa kufanya kampeni kwa muda wa siku tano tu.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Yanga SC,Wakili Ally Mchungahela wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

"Na leo baada ya mkutano huu na wanahabari nitakuwa nimezindua rasmi kampeni kuanza. Tuliongeza muda Uchaguzi wa Matawi kufanyika mpaka leo tarehe 04/07/2022, hivyo basi natangaza leo ndiyo mwisho kufanyika Uchaguzi kwenye Matawi na Matawi yote yaliyochaguliwa yalete orodha ya viongozi wao Makao Makuu ya Klabu, tawi ambalo halitaleta orodha yake viongozi wake hawataruhusiwa kufanya uchaguzi,"amesema Wakili Mchungahela.

Amesema, Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Julai 9, mwaka huu badala ya Julai 10, 2022 iliyopangwa awali ili kuruhusu majukumu mengine ya Kitaifa.

Post a Comment

0 Comments