Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Julai 11,2022


Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ranil Wickremesinghe wamekubali kujiuzulu baada ya waandamanaji kuvamia makazi yao kushinikiza viongozi hao kuachia ngazi.

Viongozi hao wamekubali kuachia ngazi baada ya waandamanaji kuvamia makazi yao huku wakichoma nyumba ya Waziri Mkuu huyo.

Waziri Mkuu Wickremesinghe amesema, ataachia ngazi mara tu baada ya Serikali mpya kuingia madarakani, na saa chache baadaye Spika wa Bunge alitangaza kuwa Rais Rajapaksa naye amekubali kujiuzulu.

Taarifa zinasema kuwa viongozi hao wakuu wa nchi hiyo hawapo kwenye makazi yao wakati huo waandamanaji walipoyazingira.

Mamia ya watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo waliwasili katika mji mkuu wa Colombo, wakimtaka Rajapaksa ajiuzulu baada ya miezi kadhaa ya maandamano kuhusu hali mbaya na usimamizi mbovu wa kiuchumi.

Hata hivyo, Rais Rajapaksa atajiuzulu rasmi Julai 13 huku Waziri Mkuu Wickremesinghe naye akikubali kujiuzulu. 

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, Spika wa Bunge la nchi hiyo, Mahinda Yapa Abeywardena amesema Rais ameamua kujiuzulu baada ya Spika kumtaarifu kuwa viongozi wa bunge walikutana na kuamua kuwa aachie ngazi.

Post a Comment

0 Comments