Huduma za kidijitali zawafurahisha wanachama wa NHIF Sabasaba

NA MWANDISHI WETU

WANANCHI na Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wamefurahishwa na uboreshwaji wa huduma za Mfuko huo ambazo kwa sasa zinapatikana kwa njia ya kielekroniki.
Hayo wameyasema kwa nyakati tofauti katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. 
Akizungumzia kuridhishwa kwa huduma hizo, Bw. Andrew Elias ambaye alifika katika banda la NHIF kwa lengo la kupata huduma ya elimu na kujiunga na huduma za Mfuko.
"Ukweli huu ni bunifu sana, nimeona ambavyo mmerahisisha mambo ambapo kwa sasa taarifa zote za uanachama zikiwemo gharama unazotumia hospitali, huduma ulizopewa na namna kadi yako iluvyotumika unazipata kupitia NHIF App haya ni mafanikio makubwa," alisema Bw. Elias.
Naye Mkazi wa Kipawa Bi. Roida Msembu ambaye alifika kwa lengo usajili, alisema kuwa gharama zinazotozwa na Mfuko zimezingatia uhalisia wa vipato vya wananchi hivyo akauomba Mfuko kufika katika maeneo mengi zaidi.

Akizungumzia ushiriki wa Mfuko katika Maonesho hayo, Meneja Uhusiano wa NHIF, Bi. Anjela Mziray alisema kuwa, Mfuko umejipanga kurahisisha zaidi huduma kupitia mitandao kutoa huduma bora na za haraka kwa wananchi lakini pia kuhamasisha wajiunge na huduma ili wawe na uhakika wa matibabu wakati wowote.
"Nawakaribisha wote wanachama na wasio wanachama kutembea banda letu la NHIF ambalo liko karibu kabisa na mlango Mkuu wa kuingilia ndani ya viwanja vya maonesho, NHIF tupo tayari kuwapa huduma ya elimu, kuwasajili na kutatua changamoto wanazokutana nazo katika kupata huduma," alisema Bi. Mziray.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news