Spika Dkt.Tulia ateta na Mkurugenzi wa BARRON GROUP,Jacqueline Kawishe

NA MWANDISHI WETU

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya BARRON GROUP,Jacqueline Kawishe.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson ( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BARRON GROUP, Jacqueline Kawishe (kulia) na Balozi wa kiatu cha shule kinachotengenezwa na kampuni hiyo, Breya Nakisiwa.Kampuni hiyo imekabidhi viatu vya watoto wa shule jozi 50 kwa Taasisi ya Tulia Trust Foundation.

Mazungumzo hayo yamefanyika Juni 30 mwaka huu , 2022 baada ya kufika kwenye ofisini za Spika wa Bunge jijini Dodoma kwa lengo la kwenda kujitambulisha na kupata ushauri wa Spika hasa kwa kutambua mchango wa Bunge katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya sekta ya uwekezaji.

Akiwa na Spika huyo wa Bunge pamoja na mambo mengine, Mkurugenzi wa Kampuni ya BARRON GROUP inayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa kiatu cha mtoto wa shule chenye chapa ya kitanzania ya BARRON, Kawishe ameelezea sababu za kuamua kutengeneza kiatu cha mtoto wa shule ambacho ni bora na kwa gharama nafuu.

"Mheshimiwa Spika wa Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tumefika ofisini kwako kwanza kujitambulisha kuwa sisi BARRON GROUP ni kampuni ya Kitanzania iliyoamua kujikita katika kutengeneza kiatu cha mtoto wa shule.

"Tulifanya utafiti na kubaini kiatu cha shule kimekuwa changamoto kwa wazazi na walezi wengi, viatu vya shule vimekuwa na gharama, lakini kwa sehemu kubwa vimekosa ubora, sisi tumeamua kuja na kiatu bora na kwa gharama nafuu,"amesema Kawishe.

Mkurugenzi huyo BARRON GROUP akiwa kwa Spika wa Bunge alikuwa ameambatana na Balozi wa kiatu hicho, Nasikiwa Byera ambapo pamoja na kujitambulisha wamekabidhi viatu vya shule jozi 50 kwa ajili ya Taasisi ya Tulia Trust Foundation.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news