IGP Sirro asema kilimo ni fursa huku akitambua mchango wa wadau

NA JUNIOR MWEMEZI-TARI

KAMANDA wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi linatambua mchango wa kilimo nchini na umuhimu wa utafiti katika kuendeleza kilimo kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) na wadau wengine katika mnyororo wa thamani.
Kamanda Sirro ameyasema hayo leo alipotembelea mabanda ya TARI ili kuona shughuli za utafiti na mchango wake katika kutekeleza Agenda 10/30 ya Kilimo ni Biashara, ambapo kilimo kinatarajia kukua kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.
"Nafarijika na maelezo yaliyotokewa kuhusu umuhimu wa kufahamu afya ya udongo kabla ya kuanza kilimo cha zao lolote ili kusaidia maamuzi ya kiasi na aina ya mbolea kulingana na zao,"amesema IGP Sirro. 

Amesema, TARI iongeze nguvu katika kuwashauri wakulima ili kuongeza uelewa na kukifanya kilimo kuwa chenye tija.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dkt. Geoffrey Mkamilo ametoa hakikisho kuwa TARI itaendelea kusambaza teknolojia za kilimo kwa wananchi na kuwasaidia kulima kilimo chenye tija.

Post a Comment

0 Comments