Rais Museveni awasili jijini Arusha,Prof.Mkenda aongoza mapokezi

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Musevani leo tarehe 21 Julai 2022 amewasili nchini Tanzania na kupokelewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof Adolf Mkenda (Mb) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Mhe. Museveni amewasili nchini kwa ajili ya kushiriki kwenye Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika kuanzia leo tarehe 21-22 Julai 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano-AICC jijini Arusha.

Post a Comment

0 Comments