Kiwanda kikubwa cha saruji (Mamba Cement) kujengwa Chalinze

NA DIRAMAKINI

IMEELEZWA uwepo wa kiwanda cha saruji kwenye Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kutasaidia kutasaidia kuiongezea mapato halmashauri na ajira kwa vijana wa mkoa huo na nchi kwa ujumla.
Akizungumza mara baada ya ziara ya Madiwani na wajumbe wa Kamati ya Uchumi ya Halamshauri hiyo kutembelea eneo la mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho cha kampuni ya Mamba Cement na mgodi wa madini yatakayotumika wakati wa uzalishaji Saruji mwenyekiti wa kamati ya Uchumi ya Halmashauri hiyo Malota Kwaga alisema mpango huo ni mzuri

Kwaga amesema kuwa, wameweka mazingira bora ya uwekezaji ili kuhakikisha mkakati wa Chalinze ya viwanda unazidi ufanikiwa.

"Lengo ni kuhakikisha kila mwekezaji anayefika Chalinze anawekeza pamoja na kila kijiji kupanga maeneo ya uwekezaji lakini Halmashauri ya Chalinze imepanga katika idara zake wataalamu wanaohusika na uwekezaji ili kuwezesha taratibu za uwekezaji zinafanikiwa kwa haraka,"amesema.

Akizungumzia uwekezaji huo wa Mgodi na Kiwanda cha Saruji cha Mamba alisema mradi huo mkubwa utakuwa mkombozi mkubw wa ajira lakini pia uongezaji wa pato la Taifa,Wilaya na vijiji vya Talawanda na Magulumatali vinavyohusika na mradi huo.

Alisema, kwa hatua waliyofikia baada ya kumaliza changamoto ya fidia ni kubwa kwani kazi zinaonekana hivyo wa kama Madiwani wanabariki mradi huokupewa baraka zote na Wizara ya Madini ili uendelee na kuleta tija kwa Taifa.

Naye Diwani wa Talawanda, Athuman Biga aliipongeza Kampuni ya Mamba Cement kwa kuwashirikiana na wanachalinze katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo miundombinu ya madarasa,zahanati na vifaa mbalimbali.

Biga amesema kwa Kata yake tu wameweza kunufaika na Kampuni hiyo katika maendeleo toka mwaka 2010 kwa kushirikiana nao katika masuala mbalimbali.

Naye Meneja mratibu wa mradi huo, Aboubakary Mlawa amesema taratibu za uhakiki zinaendelea,lakini pia shughuli za mradi zineshaaaza ikiwemo kupasua miamba na kukusanya mawe tayari ya majaribio.

Amesema, mradi huo utakuwa na utekelezaji wa awamu za upasuaji miamba,kufanya majaribia katika viwanda rafiki sambambana ujenzi wa Kiwanda katika eneo hilo kwa ajili ya utengenezaji wa Saruji.

Mlawa alisema harakati za mradi huo zilianza muda ambapo pia suala la kuwanda wataalam kutoka vijijini hapo lilianza kwa kulipia gharama za masomo kwa watoto katika kata hiyo mpaka ngazi ya chuo.

Post a Comment

0 Comments