Mambo yazidi kuwa mazuri Pemba, Rais Dkt.Mwinyi afanya jambo shuleni

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba, inayojengwa kwa Fedha za Uviko-19,kushoto kwa Rais ni Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi imefanyika Julai 26,2022.(Picha na IKULU).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mkewe Mama Mariam Mwinyi, akisoma maelezo ya jiwe la Msingi la Ujenzi wa Skuli ya Msingi Makangale Pemba, inayojengwa kwa Fedha za Uviko-19, wakati wa ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Mikoa Miwili ya Pemba.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mhandisi wa Kampuni ya Ujenzi ya Masasi Construction, Ndg. Mathias John Msila wakati akitoa maelezo ya michoro ya jengo la Skuli ya Msingi Makangale katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi huo linalojengwa kupitia Fedha za Uviko-19 na kulia kwa Rais ni mkewe wa Mariam Mwinyi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe Lela Mohammed Mussa na kushoto kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe.Salama Mbarouk.(Picha na Ikulu).
Muonekano wa Jengo Jipya la Skuli ya Msingi Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba, lililowekwa Jiwe la Msingi la Ujenzi huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi linalojengwa kwa fedha za Uviko -19.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutoa maelekezo kwa uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakati akitembelea moja ya madarasa katika jengo hilo la Skuli ya Msingi Makangale baada ya kuweka jiwe la msingi, kushoto kwa Rais ni mkewe Mariam Mwinyi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Mohammed Mussa.

Post a Comment

0 Comments