Mameya,wenyeviti wampongeza Rais Samia kwa kuibadili Dodoma

NA ANGELA MSIMBIRA, OR-TAMISEMI

MAMEYA na Wenyeviti wa Halmashauri zote nchini wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwenye Mamlaka za Serikali za mitaa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.
Pongezi hizo zimetolewa Juni 29, 2022, baada ya viongozi hao kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali katika Jiji la Dodoma. 

Miradi ambayo imetembelewa ni ule wa ujenzi wa jengo la Ikulu ya Chamwino, ujenzi wa Mji wa Serikali 'Magufuli City' na ujenzi wa jengo la Machinga.

Akizungumza kwa Niaba ya Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Mhe Japhari Juma Nyaigesha amesema, Rais Samia anapaswa kupongezwa na kushukuriwa kwa kuwaletea miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Ametumia fursa hiyo kuahidi kuhakikisha wanasimamia kwa weledi na umakini miradi inayoletwa na Serikali katika Halmashauri zao ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.

Amesema, Serikali imekuwa ikipeleka fedha nyingi kwenye Halmashauri kwa lengo la kuhakikisha miradi inatekelezwa na kukamilika kwa wakati hivyo ni jukumu lao kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akipeleka fedha nyingi kwenye halmashauri , hivyo ni wajibu wetu wastahiki mameya na wenyeviti wa halmashauri kuhakikisha tunasimamia kwa umakini mkubwa ili kumsaidia Rais aweze kutimiza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi,”amesema.

Naye Mkurugenzi wa Sera na Uratibu, Ofisi ya Waziri Mkuu Paul Sangawe amewataka viongozi hao kuwa na maono na dira kwa kutafsiri kwa vitendo ambavyo wananchi wataweza kuona na kuhakikisha wanasimamia mipango ya maendeleo kwa kutumia mapato ya ndani ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

Pia amewataka kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za viongozi wa kitaifa kwa kuhakikisha wanaeleza wananchi kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Comrade Sambala Saidi amesema wao kama viongozi Wana wajibu wa kudumisha ushirikiano baina ya Mameya, wenyeviti wa Halmashauri na Manejimenti za Halmashauri ili kuhakikisha wanaleta maendeleo kwa jamii na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.

Kwa upende wa Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Ujenzi wa Maji wa Serikali, Meshack Bandawe amesema, ujenzi wa awamu ya pili wa majengo katika Mji wa Serikali unaendelea vizuri na kuwa mkakati ni kuwa ifikapo Oktoba 2023 majengo hayo yatakuwa yamekamilika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news