Waziri Mhagama azindua huduma mpya Benki ya Stanbic inayowagusa wastaafu

NA JAMES K.MWANAMYOTO 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amezindua huduma mpya ya kibenki nchini ya Hekima Banking Tabasamu la Kustaafu inayotolewa na Benki ya Stanbic ili kutatua changamoto zinazowakabili wastaafu ikiwemo ya kutapeliwa mafao yao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kuzindua huduma mpya ya kibenki ya Hekima Banking Tabasamu la Kustaafu inayotolewa na Benki ya Stanbic kwa ajili ya kuwawezesha wastaafu kuwekeza ili kuwa na maisha mazuri baada ya kustaafu. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wanaotarajia kustaafu, wastaafu na watendaji wa Benki ya Stanbic kabla ya kuzindua huduma mpya ya kibenki ya Hekima Banking Tabasamu la Kustaafu inayotolewa na Benki ya Stanbic kwa ajili ya kuwawezesha wastaafu kuwekeza ili kuwa na maisha mazuri baada ya kustaafu. 

Mhe. Jenista mara baada ya kuzindua huduma hiyo ya kibenki jijini Dodoma, amesema huduma ya Hekima Banking maarufu kama Tabasamu la Kustaafu itawasaidia wastaafu kutoka katika mikono ya matapeli, wahuni na watu wanaoishi kwa ujanja ujanja kwa kuwalaghai wastaafu nchini. 

Waziri Jenista amesema, ana imani kuwa, hakuna mstaafu atakayeangukia kwenye mikono ya wadhalimu iwapo atapata elimu inayotolewa na Benki ya Stanbic kuhusu Huduma ya Hekima Banking almaarufu kama Tabasamu la Kustaafu. 

“Baada ya kupata elimu hii ya Hekima Banking, kila mstaafu atakuwa ametengenezewa utaratibu, miundombinu na mfumo mzuri wa kuwekeza kwenye shughuli za kiuchumi ambao utamuwezesha kuishi maisha mazuri yenye tabasamu baada ya kustaafu,” Mhe. Jenista amefafanua. 
Baadhi ya watumishi wanaotarajia kustaafu, wastaafu na watendaji wa Benki ya Stanbic wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) kabla ya waziri huyo kuzindua huduma mpya ya kibenki ya Hekima Banking Tabasamu la Kustaafu inayotolewa na Benki ya Stanbic kwa ajili ya kuwawezesha wastaafu kuwekeza ili kuwa na maisha mazuri baada ya kustaafu. 

Akizungumzia wimbi la utapeli wanaofanyiwa wastaafu, Mhe. Jenista amesema, akiwa ndiye waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma, anatoa onyo kwa matapeli wote ambao wamekuwa wakijiandaa kwa kuweka mikakati ovu ya kuwatapeli watumishi wa umma wanaotarajia kustaafu na waliostaafu. 

Kuhusu ubunifu wa Benki ya Stanbic kuanzisha huduma ya Hekima Banking kwa ajili ya kutatua changamoto za wastaafu, Mhe. Jenista ameishukuru na kuipongeza benki hiyo na kuziomba taasisi nyingine za kifedha kubuni huduma za kuwasaidia wastaafu kuwekeza mafao yao ili wawe na maisha mazuri yenye tabasamu la kudumu baada ya kustaafu. 

“Kama taasisi zote za kifedha zitasimama imara na kufanya jambo zuri kama hili la Benki ya Stanbic la kuwaandalia wastaafu huduma nzuri ya kuwa na uwekezaji sahihi kupitia mafao yao, nina imani kuwa, wastaafu wote watawezeshwa kuwa na maisha mazuri yenye tabasamu la uhakika baada ya kustaafu,” Mhe. Jenista amesisitiza. 

Aidha, ameongeza kuwa, taasisi za kifedha zikibuni huduma za kibenki kwa ajili ya kuwawezesha wastaafu kuwa na uwekezaji sahihi wa mafao yao, zitasaidia sana wastaafu kumudu gharama za maisha zikiwemo za matibabu, chakula na kusomesha kwa wastaafu ambao bado wanaendelea kusomesha watoto wao. 
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja cha Benki ya Stanbic, Bw. Omari Mtiga akieleza lengo la benki yake kuanzisha huduma ya Hekima Banking yenye kibwagizo cha tabasamu la kustaafu, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzindua rasmi huduma hiyo kwa wastaafu.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja cha Benki ya Stanbic, Bw. Omari Mtiga amesema, benki yao inayo furaha kubwa kuleta huduma ya Hekima Banking yenye kibwagizo cha tabasamu la kustaafu kwa wateja wao na watanzania kwa ujumla ili huduma hiyo iwanufaishe wastaafu wote nchini. 

Bw. Mtiga amesema kuwa, Benki ya Stanbic imeanzisha huduma hiyo ya Hekima Banking maalumu kwa wastaafu baada ya kufanya utafiti wa zaidi ya miaka miwili uliolenga kuangalia ni nini watumishi wanaotarajia kustaafu na waliostaafu wanahitaji katika eneo la uwekezaji kupitia mafao, hivyo wao kama wataalamu wamekuja na huduma hiyo ambayo ni suhuhisho la changamoto zinazowakabili wastaafu wengi nchini. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wanaotarajia kustaafu na wastaafu, mara baada ya waziri huyo kuzindua huduma mpya ya kibenki ya Hekima Banking Tabasamu la Kustaafu inayotolewa na Benki ya Stanbic kwa ajili ya kuwawezesha wastaafu hao kuwekeza ili kuwa na maisha mazuri baada ya kustaafu.

Benki ya Stanbic imebuni na kuja na Huduma ya Hekima Banking maalumu kwa wastaafu nchini, ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita za kuweka mazingira bora ya kuwawezesha wastaafu kuishi maisha mazuri baada ya kumaliza jukumu la kulitumikia taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news