Mataifa nje ya Afrika yaomba kujiunga Jumuiya ya Wazalishaji wa Almasi (ADPA)

NA MWANDISHI WETU

BAADHI ya mataifa nje ya Afrika yameomba kujiunga kama wanachama waangalizi katika Jumuiya ya Nchi Zinazozalisha Almasi Afrika (ADPA) zikiwemo taasisi zilizobobea kwenye masuala ya madini hayo.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko wakati akifunga Mkutano wa Tatu wa Dharurra wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo uliofanyika jijini Arusha na kutanguliwa na mkutano wa wataalam kutoka mataifa wanachama.

Dkt.Biteko aliongeza kwamba, suala hilo lilikuwa miongoni mwa ajenda tatu zilizojadiliwa katika mkutano huo na kwamba jumuiya hiyo imepanga kuangalia sifa na vigezo kwa nchi hizo na wakati utakapowadia italazimika kubadilisha Katiba ya jumuiya hiyo.
Lengo likiwa ni kutoa fursa kwa nchi hizo kujiunga waweze kuendelea kujengeana uwezo na kubadilisha uzoefu na nchi zilizo nje ya Afrika katika masuala ya almasi.

Pia, alisema kuwa ajenda nyingine iliyojadiliwa katika kikao hicho ni kuhusu uteuzi wa watendaji wa kudumu katika sekretatieti ya umoja huo ambapo baraza liliamua hadi kufikia katikati ya mwezi Septemba, mwaka huu watendaji hao wawe wamepatikana.
Akizungumzia utaratibu wa ajira katika umoja huo, alisema mwananchi yoyote kutoka nchi wanachama anaruhusiwa kuomba na kwa watu ambao wako nje ya mfumo wa Serikali watatakiwa kupata idhini ya Serikali.
Aliongeza kwamba, ajenda nyingine iliyojadiliwa ni kupitiwa upya na kuidhinishwa kwa Katiba ya jumuiya ambayo itawezesha kutekelezwa kikamilifu kwa matakwa ya jumuiya hiyo.
Katika hatua nyingjne, washiriki wa mkutano huo walipata fursa ya kutembelea katika hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kujionea vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo.
Katika Mkutano wa Tatu wa Dharura wa Baraza la Mawaziri, Tanzania ilikuwa nchi mwenyeji na Mwenyekiti wa sasa wa umoja huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news