RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA CHEGENI KABLA YA KULA KIAPO CHA KUWA MKUU WA MKOA WA MARA

NA DIRAMAKINI

SIKU tatu baada ya Dkt.Raphael Chegeni kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, uteuzi wake umetenguliwa.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 31, 2022 saa 1 usiku na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus ambayo imesema Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi huo na kumteua Meja Jenerali Suleiman Mzee kuchukua nafasi hiyo.

Rais Samia alimteua Dkt.Raphael Chegeni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Julai 28, 2022 kuchukua nafasi ya Ally Hapi.

Katika taarifa ya Ikulu imesema, mkuu huyo wa nchi amemtengua uteuzi wa Dkt.Chegeni huku nafasi hiyo ikichukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Jenerali Suleiman Mzee.
Meja Jenerali Suleiman Mzee

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali Suleiman Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na kutengua uteuzi wa Dkt.Raphael Masunga Chegeni,” imesema taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments