Mtibwa Sugar watwaa ubingwa U20 kwa mara nne mfululizo

NA DIRAMAKINI

MTIBWA Sugar imetwaa ubingwa wa Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuwafungia Mbeya Kwanza mabao 4-1.
Ni kupitia mtanange wa aina yake uliopigwa leo katika dimba la Azam Complex, lililopo Kata ya Chamazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Ezekiel Eusebio dakika ya 29, Ladack Chasambi dakika ya 45, Said Mkopi dakika ya 84 na Omary Suleiman dakika ya 90 waliipa heshima Mtibwa Suga.

Aidha,Mbeya Kwanza walipata bao kupitia Willie Thobias dakika ya 68 ambapo katika mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, Azam FC imeifunga Coastal Union kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 katika dimba hilo.

Post a Comment

0 Comments